• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Moshi Municipal Council
Moshi Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • History
    • Dira na Dhamira
      • Maadili ya Msingi
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi na Utamaduni
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya jamii na Ustawi wa Jamii
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Idara ya Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ununuzi na Ugavi
      • Teknolojia,Habari,Mawasiliano na Uhusiano
      • Uchaguzi
    • Muundo wa kiutawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Michezo na Utamaduni
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Videos

Madiwani wapewa Mafunzo ya Sheria Ndogo na Maadili ya Utumishi wa Umma

Posted on: February 6th, 2018

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, imetoa mafunzo ya sheria ndogondogo na maadili kwa Madiwani, lengo likiwa ni kukumbushana masuala ya maadili  na  kuimarisha ushirikiano kati ya madiwani na watendaji ili kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani.


Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna

Mghwira, alisema Mafunzo haya yatakuwa chachu kwa Madiwani na kuboresha ushirikiano kati ya madiwani na watendaji kwa nia ya kuwaletea maendeleo wakazi wa Manispaa ya Moshi.


Alisema lengo la Msingi la mafunzo hayo ni kuwawezesha Madiwani,

kupata uelewa wa sheria ndogondogo za ukusanyaji wa ada na ushuru

mbalimbali kwa ajili ya kuiwezesha Halmashauri, kupata mapato ambayo

yatafanikisha na kurahisisha utekelezaji wa shughuli za utoaji huduma

bora kwa wananchi.


Mghwira alisema Ushirikiano katika utumishi wa Umma unajengwa katika

msingi wa mgawanyo wa majukumu ya kiutumishi, na kuwataka madiwani

kutumia mafunzo hayo  kuibua ushirikiano mpya katika

utendaji kazi wakishirikiana  na watendaji wa Halmashauri .


"Waheshimiwa Madiwani, ninyi ni watumishi wa umma kwa kuwa mnashika

nafasi ambazo mnawatumikia wananchi,hivyo mafunzo haya ya sheria

ndogondogo  za ada na ushuru mbalimbali pamoja na maadili,yawezeshe

kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja kati yenu na watendaji,katika suala

zima la ukusanyaji wa mapato ndani ya Halmashauri"alisema Mghwira.


Mkuu wa Mkoa alitumia pia nafasi hiyo kuwataka madiwani kutumia

mafunzo hayo, kufanikisha shughuli za ukusanyaji wa

mapato,utayarishaji wa taarifa fasaha,sahihi na za kuaminika, ambazo

zitatumika kama rejea katika kuamua mwelekeo wa Halmashauri katika

suala zima la Mapato.


Akizungumza Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,

Bwana Michael Mwandezi, alisema  watazingatia mada zote

zitakazofundishwa kwani zitasaidia kuiwezesha Halmashauri yake  kukusanya

mapato yaliyokusudiwa.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti  baadhi ya madiwani walioshiriki mafunzo hayo,walisema mafunzo watakayoyapata yatakuwa chachu ya kuwawezesha kusimamia na

kutekeleza sheria ndogondogo za ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, pamoja na kuzingatia  maadili ya utumishi wa Umma.

Matangazo

  • TANGAZO LA USAFI WA MAZINGIRA March 28, 2018
  • TANGAZO MAEGESHO YA MAGARI March 27, 2018
  • Boda Boda na Bajaji February 02, 2018
  • Stika za Magari ya Biashara February 02, 2018
  • Tazama

Habari Mpya

  • ZAIDI YA WANAFUNZI 29,000 WA SHULE ZA MSINGI WAPEWA DAWA ZA MINYOO

    April 18, 2018
  • HALMASHAURI ZAJIFUNZA SIRI YA MAFANIKIO YA USAFI

    March 26, 2018
  • MILA KANDAMIZI ZINAWANYIMA WANAWAKE FURSA

    March 08, 2018
  • BAJETI YA ZAIDI YA SH. BILIONI 48 YAPITISHWA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019

    March 01, 2018
  • Tazama

video

Raisi akihutubia
videos

Kurasa za Karibu

Tovuti Mashuhuri

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    MOSHI MANISPAA KILIMANJARO

    Sanduku la barua: P.O BOX 318 MOSHI

    Simu: +255-027-2752906

    simu ya Mkononi: +255-027-274371/4

    Barua Pepe: md@moshimc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi